Muda mfupi kabla a mchezo wa jana kati ya Chelsea dhidi ya watford, kulitolewa taarifa kukosekana kwa Marcos Alonso kwenye mchezo huo. Haikujulikana rasmi kukosekana kwa nyota huyo, na mara baada ya mchezo huo, kocha Antonio Conte aliulizwa juu ya mchezaji huyo ambaye kwa nafasi yake ilichezwa na Davide Zappacosta ambaye alicheza kwa upande wa kushoto ikiwa ni tofauti na ilivyozoeleka kwa nyota huyo kucheza upande wa kulia.
Kocha huyo alipoulizwa juu ya Marcos alisema "Hakuna jambo kubwa kumhusu, niliamua kumpumzisha kutokana na kufululiza kucheza michezo mingi, nilimuona amechoka"
Nyota huyo mpaka sasa ameshaichezea Chelsea michezo 34 huku kwenye ligi kuu akicheza michezo 25 kati ya 26 huku akiifungia Chelsea magoli 7 ambapo kwa michezo hiyo aliyotumika bila kuwa na mbadala kamili amekuwa akitumika bila kufanyiwa mabadiliko kwa michezo mingi.

SABABU YA MARCOS ALONSO KUTOCHEZA DHIDI YA WATFORD
Share This
Tags
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment