Mara baada ya jana kuiongoza klabu yake ya Watford kupata ushindi mnono dhidi ya Chelsea, Richarlison wa Watford ambaye ni raia wa Brazil huku akiwa ana msimu mmoja tu klabuni hapo akisajiliwa kutokea klabu ya Fluminense ya nchini Brazil ambapo Chelsea imekuwa ikihusishwa kutaka pia kumnunua kabla ya nyota huyo kujiunga na Watford na hata mara baada ya kujiunga nyota huyo ametoa neno kuwahusu nyota wa Chelsea, david Luiz na Willian ambao ni wabrazil wenzake.
"Sina familia huku Uingereza, muda mwingi nimekuwa nikitumia kushinda nyumbani kwa David Luiz na tumekuwa pamoja kwa muda mrefu huku akionyesha kuwa karibu sana na mimi. Amekuwa akinifundisha vingi na tukiongea vingi, na tumekuwa tukicheza michezo ya video (video games) na mara zote huwa nachukua Watford na wao (David Luiz pamoja na Willian) wamekuwa wakichagua Chelsea, na nimekuwa nikiwafunga. Willian pia amekuwa msaada mkubwa kwangu" alisema nyota huyo
Lakini kama haujaiskia hii, jana katika mchezo huo wa Chelsea dhidi ya Watford waliokuwa nyumbani Vicarage Road, mara baada ya nyota huyo kufanyiwa mabadiliko dakika ya 65 ya mchezo alipofika kwenye benchi alianza kulia. Huenda hii ikawa kwa kuwa alishindwa kupata goli kwa maana katika mchezo wa kwanza ambapo Chelsea ilikuwa nyumbani, iliposhinda 4-2, nyota huyo alipata nafasi nyingi na kushindwa kufunga na mara baada ya mchezo huo alisema david Luiz alimwambia kuwa atazifunga timu zote Uingereza ila kamwe hatoifunga Chelsea kwa hiyo labda kulia kwake jana ni kutokana na maneno ya David Luiz.
Chelsea imekuwa ikihusishwa kumuwania nyota huyo mwenye miaka 20 kwa sasa huku mpango huo ukichochewa na Watford kumtimua kocha wake, Marco Silva ambaye inasemekana alikuwa na mahusiano mazuri na kocha huyo raia wa Ureno.

NYOTA WA WATFORD AMWAGA MACHOZI, AELEZA UHUSIANO WAKE NA LUIZ
Share This
Tags
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment