ROONEY ATOA NENO KUMHUSU ANTONIO CONTE - Darajani 1905

ROONEY ATOA NENO KUMHUSU ANTONIO CONTE

Share This
Mara baada ya mchezo wa jana wa ligi kuu kati ya Chelsea dhidi ya Watford, ulioisha kwa Chelsea kkupoteza kwa magoli 4-1, mchezaji wa klabu ya Everton ambaye kabla alikuwa mchezaji wa Manyumbu (Man utd) ametoa neno kuhusu mchezo huo, akiwa kama mmoja wa wachambuzi.

Kuhusu tatizo la Antonio Conte klabuni Chelsea
"Kila tatizo linalotokea kwenye timu, huwa ni siri na linatunzwa ndani ya klabu lakini Conte amekuwa akiyasema hadharani Huenda anafanya hivyo ili kukimbia lawama za kulalamikiwa juu ya timu nadhani anafanya hivyo kutokana na kutopewa vile anavyovitaka, wote hatujui. Lakini nadhani kuna matatizo makubwa yanaendelea ndani ya klabu" alisema nyota huyo.

Kuhusiana na kadi mbili alizozipata Bakayoko
"Nadhani zilikuwa ni kadi nyepesi sana, ingawa ndilo lilikuwa lengo la Watford. Kiwango kibovu kilionyeshwa na Bakayoko. Lakini pia timu nzima ilikuwa na mapungufu"

Kuhusu mgogoro unaoendelea kati ya bodi ya timu na kocha Antonio Conte
"Unaweza ukadhani matatizo kati ya Conte na bodi hayawadhuru wachezaji, lakini kama unavyowaona wanavyocheza katika michezo michache iliyopita, huwezi kuzani Chelsea ndio walikuwa wanacheza vile. Sijawai mkuiona Chelsea ikicheza soka lisilo na ubora kama hii kwa muda mrefu. Kuna jambo halipo sawa. Na inatakiwa kufanyike mabadiliko, Sijawai kuiona Chelsea ikicheza vibaya kama ivi kwa miaka 15"

"Mara kadhaa ilikubidi utumie akili ya ziada ili kuweza kuifunga, lakini Watford imekuwa ikipita kiurahisi na kufunga magoli. Mara baada ya Hazard kufunga goli moja, ikawa ni kama imewaamsha Watford na kuwafanya wapate urahisiwa kufunga muda wowote wakitaka" alisema mkongwe huyo mwenye heshima kubwa nchini Uingereza.


Je unakubaliana na Rooney? 

No comments:

Post a Comment