Mara baada ya kupoteza mchezo wa pili mfululizo hapo jana, Chelsea ikifungwa tena dhidi ya Watford kwa magoli 4-1 huku wiki iliyopita ikitoka kupoteza mchezo mwingine dhidi ya Afc Bournemouth. Kocha Antonio Conte ametoa neno kuhusu mchezo wa jana ambapo Chelsea ilicheza chini ya kiwango na kuruhusu kufungwa magoli matatu ndani ya dakika 8 za kuelekea mwisho wa mchezo.
"Nimefadhaika sana, kiwango chetu kilikuwa zaidi ya kibaya. Tulianza mchezo vibaya bila kuwa na utuivu, na uoga mwingi. Hatujazoea kucheza mpira kama tuliocheza jana, tulikuwa na kawaida hata kama tukipoteza mchezo basi tunakuwa tumecheza soka safi"
"Kadi mbili za njano zilizosababisha nyekundu kwa Bakayoko, haikutufanya tucheze soka safi zaidi ya kucheza ovyo kabisa. Kuongozwa kwa goli moja la penati inafanya mchezo kuwa mgumu zaidi na kuwa ngumu kurudi na kupata matokeo amzuri haswa kwa vile mmebaki wachezaji 10 uwanjani"
"Katika kipindi cha pili tulicheza soka safi. Inatakiwa uwe na uwezo kuwa na uwezo mkubwa. Lakini katika dakika 10 za mwisho tuliruhusu kufungwa magoli matatu. Kwa maana kama hiyo inamaanisha kila mtu anawajibika katika hili, mimi na wachezaji.
"Kucheza katika klabu kubwa maana yake inatakiwa uwe na hali kubwa, maana ni rahisi kucheza soka safi pale unapojiamini" alisema kocha huyo ambapo anaishuhudia Chelsea ikipoteza mchezo wake wa sita kwa msimu huu kwenye ligi kuu, michezo mingi kuliko iliyopoteza msimu uliopita ambapo Chelsea ilikuwa bingwa ikipoteza michezo mitano.

CONTE ATOA NENO, CHELSEA KUPOTEZA DHIDI YA WATFORD
Share This
Tags
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment