PL; FT, WATFORD 4-1 CHELSEA - Darajani 1905

PL; FT, WATFORD 4-1 CHELSEA

Share This

Ni mchezo ulioanza kwa kasi kwa timu za pande zote mbili uku Watford wakionekana kutengeneza nafasi nyingi za mashambulizi kabla ya Tiemoue Bakayoko aliyecheza chini ya kiwango kupata kadi nyekundu na kumfanya atolewe dakika ya 30.

Dakika kadhaa baadae, Watford wakapata penati mara baada ya mchezaji wao kuanguka ndani ya eneo la hatari na kuwafanya kupewa penati hiyo iliyoonekana kutokuwa ya halali na ndipo Watford wakapata goli la kuongoza kwa mkwaju huo wa penati. Na kufanya mpaka mpira unaenda mapumziko matokeo yakiwa 1-0, Chelsea ikiwa nyuma.

Kipindi cha pili, Chelsea ilisawazisha goli kupitia kwa Eden Hazard alipofunga mara baada ya Chelsea kuonekana kuutawala mchezo licha ya kuwa pungufu. Kwa goli hilo la Eden Hazard, matokeo yakawa 1-1.

Mara dakika kadhaa baadae wakapata goli jengine kupitia kwa nyota kutoka klabu ya Barcelona anayecheza hapo kwa mkopo, Janmaat na dakika kadhaa tena wakaongeza na mpaka mpira unaisha Chelsea ikipoteza kwa magoli hayo 4-1.

Kwa matokeo haya yanaifanya Chelsea kuwa na alama 50 huku akibakiza pengo kubwa la alama kati yake aliyepo nafasi ya nne na anayeongoza, ambao ni Mama site (Man city) kukiwa na pengo la alama 19.

No comments:

Post a Comment