Kocha wa Chelsea Muitaliano, Antonio Conte, baada ya kichapo cha ugenini cha magoli 4-1 dhidi ya Watford amesema anaiachia klabu yake kuamua hatima yake klabuni hapo kama wanafikiri hafanyi kazi nzuri.
Mabingwa hao watetezi wamepoteza michezo miwili mfululizo katika wiki na kufungwa jumla ya mabao 7 katika michezo hiyo pia wako katika nafasi ya nne kwa alama 50
"Nitabaki kuwa hapa na kujaribu kuifanya kazi yangu kwa nguvu zangu." Conte aliiambia BBC Radio 5
Muitaliano huyo alitwaa ubingwa wa ligi katika msimu wake wa kwanza, baada ya kufungwa na Bournemouth na Watford na sasa wako nyuma kwa 19 dhidi ya vinara wa ligi Manchester City.
Na kabla ya mchezo wa Jumatatu dhidi ya Watford, Conte aliomba sapoti ya uongozi na washabiki wa timu hiyo.
Wakati akiongea na waandishi wa habari mara Baada ya mchezo wa jana Conte alisema "Nina fanya kazi na inatosha lakini klabu inaweza kutoa maamuzi mengine.
Conte amebakiza mwaka mmoja na nusu (miezi 18) kabla ya kumaliza mkataba wake, alifafanua zaidi kwa kusema wachezaji wake walicheza huku wakiwa hawana utulivu na kama kocha anabeba wa lawama zote.
Kocha huyo wa zamani wa Juventus na Timu ya taifa ya Italia aliongeza kuwa inawezekana alichagua kikosi kibaya cha kuanza mchezo huo na kukubali matokeo na kuahidi kupigana zaidi katika msimu huu.
No comments:
Post a Comment