Zimesalia siku tano kabla ya kuanza michuano ya kombe la dunia itakayofanyika huko nchini Urusi na katika siku hizi zilizosalia timu za taifa zilizofudhu kucheza michuano hiyo inazitumia kucheza michezo ya kirafiki ili kupima na kuwajenga wachezaji waliowateuwa kucheza michezo hiyo.
Usiku wa jana kumechezeka michezo miwili iliyowahusisha nyota wa Chelsea ambao wataziwakilisha timu zao kucheza michuano hiyo yenye heshima zaidi duniani.
Ufaransa 1-1 Marekani
Ufaransa; Mchezo huu uliwapa nafasi nyota wote wa Chelsea, N'Golo Kante pamoja na mshambuliaji Olivier Giroud lakini usiku huo unaweza kuwa usiku mbaya kwa mshambuliaji huyo ambaye alitolewa akiwa na majeraha yanayotishia nafasi yake ya kucheza michuano hiyo akigongana kichwa na mlinzi wa Marekani, Matt Miazga
Marekani; Matt Miazga aliyepata majanga kwa kugongana na Giroud ni nyota wa Chelsea aliyetumia muda mwingi kutolewa kwa mkopo na msimu uliopita aliitumikia klabu ya Vitesse kutoka nchini Uholanzi.
Tunisia 0-1 Hispania
Hispania; Siku haikuwa nzuri sana kwa nahodha msaidizi wa Chelsea, Cesar Azpilicueta maana alikosa nafasi ya kucheza kwenye mchezo huu na badala yake alisalia kama mchezaji wa akiba.
Mchezo mwengine utakaochezwa usiku wa leo ni Austria watakaoikaribisha Brazil yenye nyota Willian Borges kutoka Chelsea.
No comments:
Post a Comment