Juzi ijumaa klabu ya soka ya wanawake ya Chelsea maarufu kama Chelsea FC Women ilikamilisha usajili wake wa kwanza katika dirisha hili la usajili la majira ya joto kwa kumsajili mlinda mlango raia wa Uingereza, Lizzie Durack mwenye miaka 24.
Mara baada ya kukamilisha usajili huo nyota huyo amefanyiwa mahojiano na kati ya maswali aliyoulizwa ni kuhusu nini kimemfanya aachane na klabu yake ya zamani ya Everton na kuamua kutimkia Chelsea.
"Ni ndoto yangu kucheza kwenye klabu kubwa kama hii lakini pia mimi kiasili ni mzaliwa wa Australia na nina marafiki zangu wengi wanaopatikana karibu na klabu hii ilipo (kusini magharibi) hivyo nimefika huku pia ili kuwa karibu nao" alisema mlinda mlango huyo.
Sasa Chelsea FC Women itakuwa na walinda mlango watatu ambao ni Hedvig Lindahl na Carly Telford pamoja na nyota huyu mpya.
No comments:
Post a Comment