CONTE KUMLETA SANCHEZ CHELSEA? - Darajani 1905

CONTE KUMLETA SANCHEZ CHELSEA?

Share This

Hizo ndizo habari zilizozagaa mara baada ya kocha Antonio Conte kuonekana akiongea jambo na nyota wa Arsenyani(Arsenal), Alexis Sanchez wakati wakiwa wanatoka vyumbani kurudi uwanjani katika mchezo uliozikutanisha Chelsea ilipomenyana na Arsenal.

Sasa leo kocha huyo aliulizwa ni jambo gani alikuwa anateta na nyota huyo walipoongea.

"Nilimwambia habari zako" alijibu Conte na kuendelea "pindi nilipokuwa kocha wa Juventud niliwai kumtaka tuungane pamoja wakati akiwa anacheza Udinese, lakini tulimkosa na akatimkia Barcelona. Nilipokutana nae kwenye mchezo ule nilimsalimia kumuonyesha kwa kiasi gani namkubali" alisema Antonio Conte.

Kuongea kwake nae kule na nyota huyo kulitafsiriwa huenda alikuwa akimshawishi waungane klabuni Chelsea ambapo kwa sasa nyota huyo anakaribia kuondoka klabuni hapo kutokana na mkataba wake kuisha mwezi Juni.

No comments:

Post a Comment