Kocha wa Chelsea, Antonio Conte amemuongelea nyota wa Chelsea, Alvaro Morata ambaye ameporomoka kwenye kiwango alichoanza nacho wakati anafika klabuni Chelsea amapo mpaka sasa hajaweza kufunga katika mechi tano mfululizo, huku mwanzo alioanza nao wengi waliamini hatoiporomka.
Kocha Conte amewapa imani mashabiki wa Chelsea juu ya nyota huyo akisema "Katika vipindi tofauti nikiwa hapa, huwa napenda kuongea na kila mchezaji, huwa naongea nao juu ya kufanya vyema mazoezini na kipi cha kufanya ili awe na kiwango bora" alisema kocha Conte.
"Morata ni mchezaji mzuri na sina tatizo nae. Kipindi kama hiki ni cha kawaida, mchezaji yoyote anaweza kupitia kipindi kama hiki. Mshambuliaji anaposhindwa kufunga, sisi mashabiki au tunaoona tunaweza kusema ana matatizo lakini muhimu kwangu kama kocha ni afanye na kupambana kwa ajili ya timu na pia atimize kile nilichomuagiza akakifanye"
"Na jambo muhimu zaidi ni kwamba, nna furaha kuwa hapa na nna furaha kuwa pamoja na Michy(Batshuayi) na hata kwa timu nzima" alimaliza hivyo kocha huyo muitaliano.
Morata amesajiliwa na Chelsea akitokea klabuni Real Madrid kwa dau la paundi milioni 60 huku mpaka sasa ameichezea Chelsea michezo 19 na kuifungia magoli 10 na kutoa pasi za magoi 4.
CONTE: NINA FURAHA NA MORATA
Share This
Tags
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment