Leo jioni Chelsea itaikaribisha klabu ya Leicester city kumenyana katika uwanja wa Stamford Bridge katika mchezo wa ligi kuu Uingereza kwa raundi ya 23, kuelekea katika mchezo huo umesikia maneno aliyasema kocha wa Leicester city?
Kocha wa klabu hiyo, Claude Puel amemwelezea nyota wa Chelsea, Eden Hazard ambaye aliwai kumfundisha nyota huyo klabuni Lille wakati Puel alipokuwa kama kocha akiifundisha klau hiyo toka mwaka 2007 mpaka mwaka 2008 kabla ya Hazard kuungana na Chelsea mwaka 2013.
"Anaweza kuwa katika ubora wake. Baada ya hapo sijui kama atabaki kuwa Chelsea au ataondoka, ana viwango vyote vya ubora vinavyoweza kumfanya akacheza klabu yoyote kubwa Ulaya. Kwa upande wangu ni mchezaji bora Ulaya, anaweaza kucheza nafasi yoyote, kulia, kushoto na hata kama mshambuliaji wa kati na hata nyuma ya mshambuliaji wa kati na akawa anarudi nyuma kuja kutafuta mipira. timu nayo imejengwa kucheza chini yake na ana ubora na thamani kubwa."
"Hata alivyokuwa na miaka 16, alikuwa na ubora kama aliokuwa nao sasa, nguvu za miguu. Haikuwa rahisi kumnyang'anya mpira pale anapokuwa nao. Anatakiwa kujifunza jinsi ligi kuu Uingereza ilivyo na hata ubora wake kwenye soka" alisema kocha huyo ambaye kabla alikuwa akiifundisha klabu ya Southampton.
MSIKIE HUYU KOCHA ALICHOKISEMA KWA HAZARD
Share This
Tags
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment