Nyota na kipenzi cha mashabiki wa Chelsea, David Luiz amekuwa akihusishwa kuondoka klabuni hapo mara baada ya kuonekana hana nafasi tena kwenye kikosi cha kwanza huku taarifa zikisema nyota huyo anataka kuondoka klabuni hapo ili kutafuta nafasi ya kuchaguliwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Brazil kitakachoshiriki kombe la dunia mwaka huu huko nchini Urusi.
Moja ya klabu alizokuwa anahusishwa nazo ni pamoja na PSG, klabu aliyokuwa anaichezea mwanzo kabla ya kurudi tena Chelsea.
Lakini kuna taarifa zinadai nyota huyo amegoma kuondoka Chelsea na anataka kuendelea kubaki hapo huku ikisemekana nyota huyo amefanya mazungumzo na kocha Antonio Conte.
No comments:
Post a Comment