Nadhani unamkumbuka vyema nyota wa zamani wa Chelsea, Florent Malouda aliyekuwa akicheza laka winga wa kulia huku akitengeneza muunganiko safi kati yake, Didier Drogba, Frank Lampard na Nicolas Anelka! Bila shaka unamkumbuka.
Alisajiliwa Chelsea mwaka 2007 na kuondoka mwaka 2013 na kuisaidia Chelsea kutwaa taji la ligi kuu Uingereza na taji la ligi ya mabingwa Ulaya.
Nyota huyo raia wa Ufaransa amekamilisha usajili katika klabu ya Diferdange inayopatikana nchini Luxembourg.
Ni kama ameshaishiwa kwa sasa kutokana na umri wake kuwa mkubwa, huwezi kuamini ni mkubwa kuliko John Terry japo mwili wake haufananii, kwa sasa ana miaka 37 na atatimiza miaka 38 mwezi Juni wakati Terry atatimiza miaka hiyo ukifika mwezi Desemba.
Amepata klabu hiyo mara baada ya kuwafata kuwaomba kufanya nao mazoezi wakati klabu hiyo ikiwa mazoezini na ndipo mara baada ya kuhudhuria mazoezi kwa siku kadhaa basi viongozi wa klabu hiyo wakaamua kumsajili kabisa.
Rais wa klabu hiyo alisema "Alikuwa anatafuta klabu ya kufanyia mazoezi nasi tukafikia nae makubaliano nasi tukakubaliana kupata ushirikiano wake mpaka mwisho wa msimu"
"Tumekuwa kwa nafasi tatu za juu kwa miaka 10 na tunashiriki katika kombe la Ulaya. Tunahitaji kushiriki tena mwaka huu, na tunahitaji Malouda atusaidie" alisema rais huyo anayeitwa Fabrizio Bei
Malouda toka aondoke Chelsea ameshavichezea vilabu kadhaa kama Trabzonspor, Metz ya Ufaransa na Delhi Dynamos na hajacheza katika timu inayoshiriki michuano yoyote mikubwa toka alipoachana na klabu ya nchini Hispania, Wadi Delga mwezi July mwaka 2016
No comments:
Post a Comment