Mpaka sasa Chelsea inaendelea kufanya mipango ili kumsajili nyota wa klabu ya As Roma ambaye ni raia wa Bosnia, Edin Dzeko licha ya usajili huo kuonekana kuwa mgumu kwa dakika za mwisho wakati kwa mwanzoni ilikuwa inaonekana ni rahisi usajili huo kukamilika.
Moja ya vyanzo vya habari nchini Italia kilidai, Chelsea imeshakubaliana na klabu yake ya jiji la Roma juu ya usajili wa nyota huyo huku kikieleza kilichobaki ni kukubaliana tu mahitaji binafsi juu ya mchezaji huyo lakini baadae moja ya viongozi wa klabu hiyo alikanusha taarifa hizo akisema hamna kilichoendelea kati ya klabu hizo juu ya uuzaji wa nyota huyo.
Sasa kuna taarifa mpya zimetoka zikidai Chelsea ipo tayari kutoa kiasi kikubwa zaidi ambapo mwanzo ilipanga kutoa paundi milioni 44 lakini kwa taarifa zilizotoka zinasema imekubali kupandisha dau mpaka paundi milioni 50 hiyo ikiwa nje ya bonasi ikimjumuisha pia na mlinzi wa klabu hiyo anayetakiwa pia na Chelsea, Emerson Palmieri.
Lakini pia taarifa zikisema Chelsea ipo tayari kumuongezea dau la mshahara nyota huyo kutoka euro milioni 4.5 kwa mwaka alizokuwa analipwa As Roma mpaka kufikia euro milioni 5.5 kwa mwaka kama atasaini Chelsea.
No comments:
Post a Comment