Huenda hii ikawa ni habari njema kwa mashabiki wa Chelsea mara baada ya gazeti moja la nchini Italia kuripoti kuwa mshambuliaji raia wa Bosnia, Edin Dzeko anayeichezea klabu ya As Roma ya nchini Italia huenda akajiunga na Chelsea muda wowote kuanzia sasa.
Jana kulitoka taarifa kutoka kwa wakala wa mchezaji huyo akisema hakuna mawasiliano yaliyofanyika kati ya Chelsea na nyota huyo lakini gazeti hilo linaripoti kuwa mwanzoni Chelsea ilipanga kuwachukua nyota wawili klabuni hapo ambao ni Edin Dzeko mwenyewe pamoja na mlinzi wa kushoto, Emerson Palmieri ambapo Chelsea ilikuwa tayari kutoa Euro milioni 50 pamoja na kuipatia klabu hiyo Michy Batshuayi akacheze hapo kwa mkopo lakini As Roma wakataka wapatiwe Euro milioni 63. Dau ambalo Chelsea hawakuwa tayari kulitoa.
Lakini baadae mara baada ya As Roma kujishauri sana na kuwaza sana wakaona wakubali dau hilo la Euro milioni 50 lakini wakamkataa Batshuayi. Inamaana Emerson na Dzeko karibuni kutua Chelsea na kuziba mapengo ambayo kocha Antonio Conte alikuwa akiyaona kwa kutaka apatiwe mlinzi mmoja wa kushoto na mshambuliaji atakayeweza kupambana na Alvaro Morata.
Hili ni dili zuri kwa Chelsea, muhimu likamilike na wachezaji hao wavae jezi za Chelsea.
No comments:
Post a Comment