Chelsea inatajwa kwa karibu kumfukuzia mshambuliaji raia wa Ufaransa, Olivier Giroud anayeichezea klabu ya Arsenyani (Arsenal) huku leo ndio ikiwa siku ya mwisho kwa dirisha la usajili la mwezi wa kwanza kufungwa.
Gazeti moja la nchini Ufaransa limeripoti kuwa Chelsea imefikia hatua za mwisho juu ya kumnasa nyota ambapo usajili wake unaweza kukamilika leo huku dau linalotajwa kuhusika katika usajili huo likiwa ni euro milioni 20 huku nyota huyo akitajwa kupewa mkataba wa miaka miwili na nusu.
Usajili huo unatajwa kuwekwa karibu na mwanamama, Marina Glanovskaia ambaye ndiye anahusika na mambo ya usajili klabuni Chelsea ambapo inaelezwa dili hilo lilikuwa likamilike au kufikiwa makubaliano kamili toka jana lakini klabu ya Arsenyani ikachelwa kukamilisha mawasiliano na Chelsea mabpo kabla Chelsea ilikuwa tayari kutoa paundi milioni 20.
Lakini pia gazeti hilo linaeleza kuwa mmiliki wa klabu ya Tottenham, Daniel Levy alifanya mawasiliano na Chelsea juu ya usajili wa mabadilishano yaani Fernando Llorente wa Tottenham aungane na Chelsea wakati wao wakimtaka Michy Batshuayi lakini Batshuayi mwenyewe hakutaka kuungana na klabu hiyo akiwa na lengo la kama akitoka klabuni Chelsea basi aende klabu ambayo itampa nafasi ya kucheza ili achaguliwe kwenye timu ya taifa ya Ubelgiji itakayosafiri kwenda kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka huu huko nchini Urusi.

No comments:
Post a Comment