Chelsea imekamilisha usajili wa nyota anayecheza kama mlinzi wa kushoto kutokea klabu ya As Roma, Emerson Palmieri ambaye ni raia wa Italia mwenye asili ya Brazil.
Chelsea imekamilisha usajili huo wa nyota huyo kwa dau la euro milioni 25 na bonasi ya euro milioni 8 kutoka klabu hiyo ya As Roma inayopatikana nchini Italia na kushiriki ligi kuu nchini humo.
Emerson alikuwa ni tayari kama mchezaji kamili wa Chelsea ambapo kilichokuwa kimebaki ni kufanyiwa vipimo vya afya na kusaini mkataba klabuni hapo.
Kama nilivyokutaarifu juzi, Emerson alikuwa ni kama tayari ashatua klabuni Chelsea kutokana na wachezaji wa nafasi klabuni hapo kutolewa kwa mkopo na kubaki mmoja ambaye ni Marcos Alonso huku Baba Rahman na Kennedy wakitolewa kwa mkopo.
Emerson ni nyota wa pili kusajiliwa katika dirisha hili la usajili ambapo kabla alisajiliwa Ross Barkley ambaye alisajiliwa akitokea klabu ya Everton kwa dau la paundi milioni 15.
Karibu Emerson Palmieri.
No comments:
Post a Comment