ARSENAL INAMHITAJI ANTONIO CONTE - Darajani 1905

ARSENAL INAMHITAJI ANTONIO CONTE

Share This
Nyota wa zamani wa klabu ya Arsenyani (Arsenal), Stewart Ian Robson ambaye kwa sasa anafanya kazi ya uchambuzi wa michezo  kwenye vipindi vya Tv na redio amemuongelea kocha wa Chelsea akisema ni mmoja ya makocha bora na wanaofaa kuirithi nafasi ya kocha wa sasa klabuni Arsenyani, Arsene Wenger endapo ataondoka.

Mkongwe huyo wa soka amesema "Conte ni kocha bora zaidi. Akienda kwenye timu au haswa akifika pale Arsenal atawafanya wachezaji wafanye kile anachokitaka wachezaji wake wakifanye"

"Wachezaji watajua ni kipi kocha anakitaka, na wapi kuna mshimo kwenye klabu ili waweze kuyafukia. Naamini Conte atakuwa ni chaguo sahihi kuwa kocha wa Arsenal" alisema mchambuzi huyo.

Klabu hiyo, juzi ilipoteza taji lake la kwanza mara baada ya kupokea kichapo kutoka kwa klabu ya Mama site (Man city) katika michuano ya Carabao Cup.

No comments:

Post a Comment