MSIKIE MOURINHO ALICHOKISEMA KUHUSU WILLIAN - Darajani 1905

MSIKIE MOURINHO ALICHOKISEMA KUHUSU WILLIAN

Share This
Kocha wa klabu ya manyumbu (Man utd) ambaye alishawai kuifundisha Chelsea, Jose Mourinho aliiongoza vyema klabu yake kupata ushindi wake wa pili dhidi ya klabu yake ya zamani hapo juzi, akiiongoza kupata ushindi wa magoli 2-1 wakati klabu yake ilipokuwa nyumbani. Mara baada ya mchezo huo, kocha huyo alifanyiwa mahojiano na waandishi wa habari akiulizwa juu ya mchezo huo na katika mahojiano yake alimtaja nyota wa Chelsea, Willian Borges ambaye ndiye alikuwa mfungaji wa goli pekee la Chelsea.

"Je unataka kuongea kuhusu Willian? Uwezo wa juu na ubora mkubwa, ni mchezaji wa kiwango cha juu. Katika timu yake ya taifa (Brazil) hakunaga mchezaji mbovu, kila mchezaji anajua soka"

"Kocha wake (Kwa timu ya taifa, Tite)  anakuwa bora kwa kuwa na wachezaji bora, naamini watafanya makubwa sana huko Urusi (kwenye kombe la dunia)" alisema kocha huyo akitoa sifa kedekede kwa nyota huyo.

Willian na Mourinho waliwai kuwa pamoja klabuni Chelsea na kufanikiwa kutwaa mataji mawili ambayo ni ligi kuu Uingereza kwa msimu wa 2014-2015 pamoja na taji la kombe la ligi kabla ya kocha huyo kuondoka. Willian alishawai kukiri kuwa kocha huyo aliwai kuonyesha nia ya kumtaka mara baada ya kuungana na klabu yake hiyo mpya ya jijini Manchester.

No comments:

Post a Comment