NYOTA WA CHELSEA KWENYE KIKOSI BORA - Darajani 1905

NYOTA WA CHELSEA KWENYE KIKOSI BORA

Share This
Kwa kawaida kila kunapokaribia au kufikia mwisho wa michuano fulani, huwa kunachaguliwa wachezaji 11 walioshiriki michuano hiyo na kuonyesha kiwango cha hali ya juu na hivyo kutengenezwa kikosi kimoja kinachoitwa kikosi bora cha michuano hiyo, huku pia akichaguliwa na kocha mmoja.

Michuano ya kombe la ligi ambayo msimu huu yalikuwa yakijulikana kama Carabao Cup yamemalizika hapo siku ya jumapili na kuwashuhudia Mama site (Man city) wakiibuka kuwa mabingwa wapya wa michuano hiyo mara baada ya kuibamiza Arsenyani (Arsenal) katika mchezo wa fainali. Na kama ilivyoada, uongozi waliokuwa wanasimamia michuano hiyo wakatoa kikosi cha wachezaji bora ambao katika kikosi hicho kimemjumuisha pia nyota wa Chelsea, Eden Hazard kama mmoja wa wachezaji hao 11.

Kikosi kipo hivi;
Kipa: Will Norris (Wolverhampton Wanderers)
Beki: Joe Bryan (Bristol City)
Beki: Aden Flint (Bristol City)
Beki: Rob Holding (Arsenal)
Kiungo: Eden Hazard (Chelsea)
Hazard alicheza kwa kiwango cha hali ya juu katika mafanikio ya Chelsea katika michuano hiyo ambapo winga huyo alihusika vyema katika mchezo dhidi ya Nottingham Forest akitengeneza magoli mawili katika ushindi wa mabao 5-1. Alihusika vyema pia katika goli la mwisho lililofungwa na Alvaro Morata dhidi ya Afc Bournemouth katika ushindi wa mabao 2-1 na kusababisha Chelsea kuisaidia Chelsea kufudhu kucheza dhidi ya Arsenyani (Arsenal) katika hatua ya nusu fainali.
Kiungo: Jack Wilshere (Arsenal)
Kiungo: Kevin De Bruyne (Manchester City)
Kiungo: Bernardo Silva (Manchester City)
Mshambuliaji: Islam Slimani (Leicester City)
Mshambuliaji: Josh Murphy (Norwich City)
Kocha: Lee Johnson (Bristol City)

No comments:

Post a Comment