ZIDANE AMJIBU MORATA KUHUSU MADRID - Darajani 1905

ZIDANE AMJIBU MORATA KUHUSU MADRID

Share This
Nyota wa Chelsea ambaye ni raia wa Hispania, Alvaro Morata amejibiwa na kocha wake wa zamani, Zinedine Zidane aliyekuwa nae klabuni Real Madrid ambapo huko ndipo alipotokea kabla ya kusajiliwa na Chelsea kwa dau la paundi milioni 60 katika dirisha kubwa lililopita.

Nyota huyo alifanyiwa mahojianao na chombo kimoja na kumlalamikia kocha wake huyo wa zamani ambaye ni raia wa Ufaransa, akisema hakuwa akilalamika kutumika kwake kama mbadala halikuwa tatizo kwake kutokana na kutambua kuwa Real Madrid ni klabu kubwa duniani ni ngumu kuwa na uhakika wa kutuimika kama mshambuliaji nambari moja. Lakini pia akisema kutokuchezeshwa kwake katika michezo kama dhidi ya barcelona, Sevilla, Atletico Madrid na Atletico Madrid halikuwa jambo kubwa kwake, lakini pia akikosa kucheza hatua yoyote ya mtoano katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.

Nyota huyo amepata majibu kutoka kwa kocha wake huyo ambaye amekuwa na msimu mbaya klabuni hapo akiwa hana uhakika wa kuendelea na kibarua chake, kocha Zinedine Zidane ametoa majibu akisema "Kwangu hakunaga mchezo mdogo, kila mchezo ni mkubwa na mpaka mchezaji kupata nafasi ya kucheza maana yake anatakiwa kucheza mchezo huo maana naye ni mchezaji mkubwa"

"Tuna mchezo dhidi ya PSG katika mtoano, mchezo ambao kila mchezaji anataka kucheza, lakini sisi kama timu hatuwezi kumchezesha kila mchezaji kwenye mchezo huo" alimaliza kwa kusema hivyo mfaransa huyo mwenye asili ya kiarabu. Real Madrid mpaka sasa imebakiwa na mshambuliaji Karim Benzema ambaye mpaka sasa ameshafunga magoli manne wakati Alvaro Morata mpaka sasa ameshafunga magoli 12.

No comments:

Post a Comment