TATIZO LINALOITESA CHELSEA NA DUNIA YA SOKA NI HILI - Darajani 1905

TATIZO LINALOITESA CHELSEA NA DUNIA YA SOKA NI HILI

Share This
Nyota wa Chelsea, Alvaro Morata ametoa tuhuma juu ya kocha wake wa zamani wa Real Madrid, Zinedine Zidane ambaye alimuuza kuja Chelsea ktika dirisha kubwa la usajili lililopita ambapo alitua klabuni hapa kwa dau la paundi milioni 60. Mpaka sasa ameshaifungia Chelsea magoli 12. Kusoma tuhuma alizozitoa kwa kocha wake huyo, bonyeza hapa.

Ila katika taarifa hii au makala haya kuna jambo nataka nikupe ili nawe ulitafakari ujiulize na kuona umbali utakaoweza kuliona au kulitafakari hili

Darajani 1905 inashangazwa kwanini katika kipindi hiki kuna wachezaji wengi wanatua Chelsea au kuichezea sio kwa vile wamefika Chelsea kwa mapenzi, ila wmefika hapo wakiwa kishingo upande. Olivier Giroud aliwai kukaririwa akisema hakutaka kuondoka Arsenyani (Arsenal) lakini aliondoka hapo akitaka nafasi ya kucheza kombe la dunia akiwa na timu ya taifa ya Ufaransa, nyota huyo mwenye miaka 31 alihojiwa na kusema kocha wake wa timu ya taifa ya Ufaransa, Deschamps alimwambia aondoke klabuni hapo ili kutafuta nafasi katika vilabu vyengine kama anahitaji kucheza kombe la dunia.

Thibaut Courtois nae anasema anacheza Chelsea lakini moyo wake upo Madrid, mahali ambapo familia yake inaishi huko na hivyo kumsababisha asuesue kwenye kusaini mkataba mpya licha ya kuwekewa mpaka dau kubwa la mshahara ambalo lingweza kumfanya awe mlinda mlango anayelipwa zaidi.

Lakini Darajani 1905 haioni maneno kama haya ungeyasikia kwa magwiji waliowai kupita klabuni hapo kama Frank Lampard, Didier Drogba, Michael Ballack na wengine. Lakini pia kwa kuwa nimesema kwa kipindi hiki acha tusikumbushie ya Eden Hazard, maana nae aliwai kukaririwa akisema hakutaka kutua Chelsea, lakini alitua mara baada ya kufanya mawasiliano na Didier Drogba ambaye kwa mwaka huo wa 2012 ndio alitoka kuisaidia Chelsea kutwaa taji la ligi ya mabingwa barani Ulaya, kila mtu alikuwa akimuita shujaa.

Kwa Chelsea hii ya sasa, ni wachezaji wengi wanacheza sio kwa vile ni mashabiki wa timu ila kwa kuwa wanahitaji kucheza na kupita klabuni hapo kisha kutimkia klabu nyengine.

Labda huenda sio tatizo la Chelsea tu ila kwa soka la kisasa ni wachezaji wachache wanaichezea klabu kwa vile wanahitaji mshahara au hata kwa kutokana na sababu zao binafsi ambazo labda sisi hatuzijui na ndio baadae unakutana na haya mambo yaliyopo kwa sasa klabuni Chelsea.

Mwandishi wa habari wa ESPN, Alejandro Mario aliwai kukaririwa akisema klabuni Chelsea kuna mgomo wa wchezaji ambapo kuna matabaka mawili ambapo kuna wale wanaotaka kuwa chini ya kocha wa sasa wa Antonio Conte na wengine wakitaka aondoke. Ni ngumu kesi kama hizi kuzisikia miaka ya magwiji hao kwa miaka kadhaa iliyopita.

No comments:

Post a Comment