HAZARD AWA BORA BARANI ULAYA - Darajani 1905

HAZARD AWA BORA BARANI ULAYA

Share This
Mtandao wa  CIES Football Observatory ambao huwa unatoa takwimu juu ya mchezo wa soka umetoa taarifa na takwimu juu ya wachezaji wanaoongoza kwa kukokota mpira katika ligi kuu tano bora barani Ulaya ambapo zinajumuisha ligi kuu Uingereza (Premier League), ligi kuu Hispania (La Liga), ligi kuu Italia (Serie A), ligi kuu Ufaransa (Ligue 1) pamoja na ligi kuun ya nchini Ujerumani (Bundesliga) ambazo ndizo zinazotajwa kuwa ligi bora tano barani humo.

Nyota wa Chelsea, Eden Hazard ambaye ni raia wa Ubeligiji mwenye miaka 27 anatajwa kuwa mchezaji anayeongoza kwa kukokota mpira ukijumuisha kwenye ligi hizo bora barani humo. Eden Hazard amekuwa juu ya nyota wanaotajwa kuwa bora kama Neymar na Lionel Messi katika ukokokotaji mpira akiwa na wastani wa kukokota 6.4 ambazo ni sawa na 75% kwa kila mchezo.

Hongera kwake Eden Hazard.

No comments:

Post a Comment