BAKAYOKO KUREJEA UWANJANI - Darajani 1905
Kupitia mtandao wa Instagram, kiungo wa Chelsea, Tiemoue Bakayoko ametuma ujumbe wa video ukimuonyesha akifanya mazoezi kujiandaa kurejea uwanjani mara baada ya kukaa nje kwa muda mrefu.

Nyota huyo amekuwa akisumbuliwa na majeraha yaliyomfanya kuwa nje kama alivyokaririwa kocha wa Chelsea, Antonio Conte akitoa taarifa juu ya mchezaji huyo kuwa nje kutokana na majeruhi yaliyompata tangu alipocheza mchezo wake wa mwisho dhidi ya Watford na kutolewa nje kwa kadi nyekundu.
Nyota huyo anaweza akaungana na wachezaji wenzake muda wowote kuanzia sasa ili kuyatimiza majukumu yake.

No comments:

Post a Comment