CHELSEA YAZIDI KUMSHAWISHI HAZARD - Darajani 1905

CHELSEA YAZIDI KUMSHAWISHI HAZARD

Share This

Chelsea imejaribu kumshawishi winga wake klabuni hapo, Eden Hazard ili asaini mkataba mpya katika vipindi tofauti tofauti kabla ya kutoka taarifa kuwa nyota huyo amekataa kusaini mkataba huo wa kuendelea kubaki Chelsea kwa miaka mingine huku baba yake akikaririwa akisema kugoma kwa nyota huyo ni kutokana na nyota huyo kutaka kujiunga na Real Madrid ambapo baadae Hazard mwenye miaka 27 kwa sasa kukana na kusema anataka kubaki Chelsea.

Mkataba wake wa sasa na Chelsea unaisha mwaka 2020, na Real Madrid wanamtazama mbelgiji huyo kama chaguo lao la kwanza kumsajili katika dirisha kubwa la usajili huku kiasi cha paundi milioni 124 kikitajwa kuhusika katika biashara hiyo.

Kutokana na hali hiyo, Chelsea imempa ofa nono mchezaji huyo ili asaini mkataba mpya, ambapo ofa hiyo inatajwa kufikia paundi 300,000 kwa wiki ambao ni mshahara wake.

Je una maoni gani katika hili?

No comments:

Post a Comment