CHELSEA KUMNASA NYOTA WA UFARANSA - Darajani 1905

CHELSEA KUMNASA NYOTA WA UFARANSA

Share This
Klabu ya Chelsea imekuwa ikitajwa kumtaka nyota wa klabu ya OGC Nice, Michae Serri anayeichezea klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya nchini Ufaransa maarufu kama Ligue 1 katika dirisha dogo la mwezi januari lililopita, lakini ikashindwa kuonyesha nia yake ya dhati kumnyakua nyota huyo na kumfanya kuendelea kubaki klabuni hapo.

Lakini sasa juhudi za kutaka kumnasa kiungo huyo zinaonekana kuanza mara baada ya Chelsea kuwatuma watu wake ili kwenda kumtazama nyota huyo anayeweza kucheza kama kiungo akiatazamiwa kuja kutengeneza muunganiko mzuri na N'golo Kante ambapo Tiemoue Bakayoko anaonekana kushindwa kuendana na mfumo klabuni hapo.

Chelsea iliwatuma watu wake kumtazama nyota huyo raia wa Ivory Coast katika mchezo wa jana ambapo klabu hiyo ilimenyana na Lokomotiv Moscow katika mchezo wa kombe la Europa League ambapo klabu yake ilipoteza mchezo huo kwa magoli 3-2.

Michael Serri mwenye miaka 26 na ameshaichezea Nice michezo 31 huku akiifungia goli moja na kutengeneza mengine manne.

Je anafaa kutua Chelsea?

No comments:

Post a Comment