HABARI MUHIMU KUELEKEA CHELSEA vs HULL CITY - Darajani 1905

HABARI MUHIMU KUELEKEA CHELSEA vs HULL CITY

Share This

Chelsea leo itakuwa nyumbani kucheza mchezo wa kombe la FA dhidi ya Hull city  kwenye hatua ya 16 bora au raundi ya tano ambapo mshindi wa hatua hiyo atafanikiwa kufudhu kucheza hatua ya robo fainali.

Chelsea itashuka katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu zuri ya kushinda michezo mitano dhidi ya klabu hiyo katika michezo ya mwisho kukutana na klabu hiyo.

Hapa nakuletea habari muhimu kabla ya kuelekea katika mchezo huo;
Chelsea; Tiemoue Bakayoko, Ross Barkley na David Luiz ndio wataukosa mchezo wa leo kutokana na kuwa na majeruhi. Huku Alvaro Morata na Andreas Christensen wakirudi vyema kutoka kwenye majeruhi yaliyowafanya kukosa mchezo.

Habari kuhusu Marcos Alonso na Olivier Giroud ambaye alikanyagwa kichwani kwenye mchezo uliopita dhidi ya West Brom, wote wanaonekana kuwa sawa na wanaweza kuanza kwenye mchezo wa leo.

Hull city; Greg Luer na Abel Hernandez wote wataukosa mchezo wa leo kutokana na majeruhi, huku Ola Aina na Fokoyi Tomori nao wakiukosa mchezo wa leo kutokana na Chelsea kuwa ni klabu yao na huko wapo kwa mkopo wakati Seb Larsson akiukosa mchezo huu kutokana na adhabu.

Mwamuzi; Andre Mariner ndiye atakuwa mwamuzi wa mchezo wa leo huku akielekea kutimiza mchezo wa 40 akiwa mwamuzi ambapo Chelsea ilikuwa uwanjani, huku akihusika katika mchezo ambao Chelsea ilishinda 3-1 dhidi ya Huddersfield lakini pia akihusika katika mchezo ambao Chelsea ilipoteza mbele ya Crystal Palace kwa magoli 2-1.

Rekodi; Chelsea iliibamiza klabu hii magoli 6-0 mwaka 1999 na imekuwa na rekodi nzuri dhidi ya klabu hii ambayo inashiriki ligi daraja la kwanza nchini Uingereza maarufu kama Championship.

Mechi zilizopita;
Chelsea; LWLLW
Hull city; LWDLW

Muda; Saa 11:00 Usiku (Saa 23:00) kwa saa za Afrika Mashariki

No comments:

Post a Comment