CHELSEA YAONGOZA KWA LEWANDOWSKI - Darajani 1905

CHELSEA YAONGOZA KWA LEWANDOWSKI

Share This
Klabu ya Chelsea inatajwa kumfukuzia mshambuliaji wa klabu ya FC Bayern Munich ya nchini Ujerumani, Robert Lewandowski ambaye kwa sasa ana miaka 29. Chelsea inatajwa kumfukuzia mshambuliaji huyo raia wa Poland huku ikitajwa kuwa ndio klabu ya kwanza kukaribia kumnasa nyota huyo.

Nyota huyo anatajwa kukaribia kutua Chelsea, kutokana na klabu hiyo kukosa mshambuliaji wa kutumainiwa lakini usajili huo ukichangizwa kwa kiasi kikubwa na wakala aliyeajiriwa na nyota huyo hivi karibuni anayejulikana kwa majina kama Pini Zahavi ambaye wakala huyo anatajwa kuhusika kwa kiasi kikubwa pale mmiliki wa sasa wa Chelsea, Roman Abramovich alipoinunua klabu hiyo kutoka kwa mmiliki wa zamani wa klabu hiyo, Ken Bates.

Zahavi anatajwa ndiye atakayechochea ukaribu wa mshmabuliaji huyo na klabu ya Chelsea kutokana na ukaribu uliopo kati yake na mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich.

Darajani 1905 inaamini huyu sio chaguo sahihi kwa Chelsea kama itakuwa na malengo naye ya muda mrefu kutokana na muda wake wa kucheza soka la ushindani kuelekea kuwa mwisho. Kwa sasa ana miaka 29 wakati itakapofika mwezi Agosti atakuwa anatimiza miaka 30, je ataweza kutoka kwenye ligi ya Ujerumani ambayo ushindani wake ni tofauti na ilivyo ligi kuu Uingereza ambayo ndiyo ligi yenye ushindani wa hali ya juu na akaja kuipa mafanikio Chelsea?

Ingawa atakuwa na faida kwa Chelsea kutokana na uzoefu aliokuwa nao haswa kwenye michuano mikubwa kama klabu bingwa Ulaya lakini kutokana na umri wake inamaanisha hatokuwa na faida kubwa kama Chelsea itakapowasajili wenye umri mdogo.

No comments:

Post a Comment