WALIOCHEZA CHINI YA KIWANGO, Man Utd 2-1 CHELSEA - Darajani 1905

WALIOCHEZA CHINI YA KIWANGO, Man Utd 2-1 CHELSEA

Share This
Katika michezo 15 iliyopita dhidi ya Manyumbu (Man utd), Chelsea inapoteza mchezo wa pili, mchezo ambao Chelsea ilitengeneza nafasi nyingi na kumiliki mpira kwa kiasi kikubwa, ila kukosekana kwa utulivu katika umaliziaji haswa kipindi cha kwanza kumeifanya Chelsea kukosa ushindi muhimu siku ya leo.

Hapa nakuletea orodha ya wachezaji ambao hawakucheza vizuri katika mchezo wa leo na kuifanya Chelsea ishindwe kugombania nafasi katika timu nne zilizopo kwenye msimamo wa ligi kuu kabla ya mchezo ujao dhidi ya Mama site (Man city).





Alvaro Morata-5/10
Hakuonekana kuwa sawa, huku akikosana kwenda sawa na hali ya mchezo waliokuwa nayo wenzake katika safu ya ushambuliaji, hakuonekana kuwa na madhara sana kwa wapinzani huku kuhusika zaidi kwenye mashambulizi na timu kumiliki mpira kuwa mbovu. Ilitakiwa kocha amfanyie mabadiliko.

Danny Drinkwater-5/10
Amecheza soka safi kwa nafasi yake kama kiungo, akizunguka na kucheza soka safi, lakini hakuonekaka kuwa kiungo mwenye kutimiza majukumu yake ipasavyo kwa kuwa hatari zaidi kwenye safu a ushambuliaji na nafasi ya ulinzi.



Marcos Alonso-5/10
Alikuwa akijitahidi kupanda mbele ili kusaidia mashambulizi katika safu ya ushambuliaji ingawa hakufanikiwa huku akionekana kushindwa kwenda na kasi ya mchezo na kufanya ukabaji (marking) mbovu na kumruhusu Lukaku apige pasi akiwa na nafasi iliyomfikia Lingard na kufunga goli la pili.

Victor Moses-5/10
Alikuwa sawa katika nafasi ya ulinzi, lakini hakutendea haki nafasi yake kama winga kwa kushindwa kutengeneza pasi ndefu (cross) ambazo zingeweza kusababisha madhara kwa wapinzani huku akipata nafasi za kufanya hivyo naye akashindwa kutimiza.






No comments:

Post a Comment