PL; Man utd 2-1 CHELSEA - Darajani 1905

PL; Man utd 2-1 CHELSEA

Share This

Kocha wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho ambaye kwa sasa ni kocha wa Manyumbu (Man utd) anapata ushindi wa pili kati ya michezo mitano aliyokutana dhidi ya Chelsea iliyochini ya Antonio Conte.

Ni matokeo mabaya kwa Chelsea maana hii inamaanisha inakaa nje ya klabu nne za juu katika msimamo wa ligi kuu Uingereza ambapo kwa sasa inashika nafasi ya tano katika msimamo huo huku wakiwa na alama 53.

Chelsea ilianza mchezo kwa kumiliki mchezo kwa asilimia kubwa huku Willian akiipatia goli la kwanza mnamo dakika ya 32 kabla ya wapinzani kuchomoa kupitia Romelu Lukaku aliyefunga goli hilo dakika ya 39. Mpaka kuisha kipindi cha kwanza mpira uliisha kwa suluhu ya 1-1.

Kipindi cha pili, haikuwa sawa mpaka kuruhusu goli la pili kupitia kwa Jesse Lingard na kuipatia klabu yake ushindi wa 2-1.

Darajani 1905, tunaona haikuwa na haja ya kumtoa Eden Hazard na kumuacha Alvaro Morata aliyeonyesha hakuwa katika hali ya mchezo. Chelsea inaonekana kuwa hatari sana ikicheza na washambuliaji watatu ambao ni Pedro, Hazard na Willian kama ilivyokuwa kwenye mchezo uliopita dhidi ya Barcelona. Kutolewa kwa Eden Hazard kulimaanisha wapinzani walikuwa na nafasi kubwa ya kupanda zaidi na kuja kusaidia mashambulizi.

Ila yote kwa yote, huu ndio mpira na haya ndio matokeo ingawa mashabiki wa Chelsea tunaumiaga sana kufungwa na Manyumbu.

No comments:

Post a Comment