KITAMBO; UNAIKUMBUKA HII YA RAMIRES - Darajani 1905

KITAMBO; UNAIKUMBUKA HII YA RAMIRES

Share This
Mara baada ya Chelsea kupata ushindi katika mchezo wa kwanza uliochezwa Stamford Bridge dhidi ya Barcelona mwaka 2012, ambapo Chelsea ilipata ushindi wa bao 1-0 katika michuano ya klabu bingwa Ulaya, safari ikaanza kwa Chelsea kusafiri mpaka nchini Hispania katika uwanja wa Barcelona maarufu kama Camp Nou ambapo hukoilihitaji kupata ushindi au suluhu ya iana yoyote ili ifanikiwe kufdhu kucheza mchezo wa fainali katika jiji la Munich.

Chelsea ilifika nchini Hispania, na tayari wakawa wamesharuhusu kufungwa magoli mawili, ambapo ilishaonekana tayari Barcelona wameshafanikiwa kufudhu kucheza fainali kabla ya kiungo wa Chelsea, Ramires kufunga moja ya magoli bora kuwai kufungwa kwa hatua hiyo ya nusu fainali ya klabu bingwa Ulaya.

"Niliupokea mpira, kisha nikatoa pasi kwa Frank Lampard, ambaye mwenyewe alipga chenga kidogo, nami nikatumia udhaifu wa mabeki wa Barcelona kwa kukimbia na kutafuta nafasi, naye Lampard aliniona akanipasia pasi ndefu kidogo, nililazimika kuongeza kasi ili kuuwai mpira. Ndipo nikamuona Valdes (kipa wa kipindi iko wa Barcelona) anasogea kunifata. Nikawaza kwa haraka kwamba ili nifunge sehemu kama hii, njia ni moja tu, kupiga mpira juu ya kipa, nami nikauchop kwa chini"

"Nilifurahia sana kwa goli kama lile, baada ya kuuchop kwa chini nikaenda kushangilia, lakini nikageuka tena kuangalia kama lingekuwa ni goli, nilipoona mpira umegusa nyavu nikaendelea kushangilia. Kikubwa nilihokisikia ni kelele za mashabiki wa Chelsea, uwanja mzima ulikuwa kimya ila zilisikika kelele za mashabiki wa Chelsea tu. Lilikuwa ni jambo lenye mvuto kwangu" alisema nyota huyo ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Jiangsu Suning ya nchini China.

No comments:

Post a Comment