Chelsea inapata ushindi wake muhimu katika uwanja wake wa Stamford Bridge, ikiibamiza West Bromwich kwa jumla ya magoli 3-0, magoli yakifungwa na Eden Hazard aliyefunga mara mbili huku jengine likifungwa na Victor Moses.
Chelsea inapata ushindi huu muhimu ambao unawapatia alama tatu muhimu na kufanikiwa kurudi kwenye nafasi ya nne mara baada ya kushushwa na Tottenham iliyofikisha alama 52 mara baada ya kuifunga Arsenyani (Arsenal) katika mchezo wao wa jumamosi.
Chelsea sasa inafikisha alama 53 ambazo zinamaanisha kuachwa alama 19 na klabu ya Mama site (Man city) walioko kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ambao wenyewe wana alama 72.
Eden Hazard ndiye aliyefungua karamu ya magoli, akifunga goli safi mara baada ya kupewa pasi safi na mshambuliaji mpya wa Chelsea, Olivier Giroud ambaye ndiye alikuwa akicheza mchezo wake wa pili kwa Chelsea, lakini pia akicheza mchezo wake wa kwanza akiwa kama mmoja wa kikosi cha kwanza.
Mpaka mpira unaenda mapumziko, Chelsea ilikuwa mbele kwa ushindi wa bao 1-0.
Kipindi cha pili kilianza na kushuhudiwa Giroud akitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Alvaro Morata ambaye alihusika katika shambulizi la goli la pili mara baada ya Victor Moses kutoka na mpira pembeni na kumpasia Cesc Fabregas aliyetaka kuonganisha pasi hiyo kwa kupiga kisigino ili kumpasia Morata aliyekuwa kwenye eneo la hatari la klabu hiyo ili kufunga lakini mlinzi wa West Brom akagongwa na mpira ule uliomkuta Moses na kuonganisha moja kwa moja. Na kufanya matokeo kuwa 2-0.
Dakika kadhaa tena baadae, Eden Hazard akatumia ufundi wake akipokea pasi safi kutoka kwa Morata na kukokota mpira kidogo kabla ya kupiga shuti lililomfanya kipa wa klabu hiyo kubaki akiuangalia tu mpira ukizama kwenye nyavu zake. Nakufanya matokeo kuwa 3-0 mpaka mpira unaisha.
No comments:
Post a Comment