ABRAMOVICH AMTAKA GWIJI WA CHELSEA KUWA MRITHI WA CONTE - Darajani 1905

ABRAMOVICH AMTAKA GWIJI WA CHELSEA KUWA MRITHI WA CONTE

Share This
Kocha wa Chelsea, Antonio Conte anatajwa kuondoka klabuni hapo mara baada ya msimu huu kuondoka huku klabu ya PSG ya nchini Ufaransa ikitajwa kuiwania saini yake kutokana na kuvutiwa na kocha huyo mara baada ya kuiongoza vyema Chelsea kutwaa taji la ligi kuu katika msimu wake wa kwanza klabuni hapo.

Kuna majina mengi yanatajwa kuwa mrithi wa kocha huyo klabuni Chelsea ambapo moja ya majina yaliyoingia kwenye orodha hiyo ni kocha wa klabu inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Uingereza (Championship), Slavisa Jokanovic ambaye alishawai kuichezea klabu ya Chelsea.

KOcha huyo ambaye aliwai kupita Chelsea kama mchezaji katika miaka 2000 mpaka mwaka 2002 aliichezea Chelsea michezo 39 ambaye alikuwa akicheza kama kiungo mabaji hajawai kuifundisha klabu yoyote ya ligi kuu Uingereza na sasa ndiye anatajwa kuwaniwa na mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich ili atue klabuni hapa.

No comments:

Post a Comment