CHELSEA YASHINDA VITA YA KUMNASA MBRAZILI - Darajani 1905

CHELSEA YASHINDA VITA YA KUMNASA MBRAZILI

Share This

Klabu ya nchini Italia, Lazio inatajwa kuingia makubaliano na Chelsea ili kumuuza nyota wake raia wa Brazil anayeichezea klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu nchini Italia maarufu kama Serie A.

Lazio inatajwa kuwa tayari kumuuza Felipe Anderson mwenye miaka 25 kwa sasa ili ajiunge na klabu ya Chelsea ifikapo msimu wa usajili wa dirisha kubwa huku dau linalotajwa kutumika katika usajili huo likiwa ni paundi milioni 20.

Felipe Anderson amekuwa akitajwa kutakiwa na klabu nyingi barani Ulaya ambapo klabu kama Napoli na Manchester united zimewai kutajwa kumuwania nyota huyo bila mafanikio, na sasa Chelsea ndio inatajwa kumfukuzia huku ikionekana imefikia hatua za mwisho za kumnasa mbrazili huyo.

No comments:

Post a Comment