CHELSEA KUMGOMBANIA NYOTA KUTOKA UFARANSA - Darajani 1905

CHELSEA KUMGOMBANIA NYOTA KUTOKA UFARANSA

Share This
Klabu ya Chelsea inatajwa kuingia sokoni na kugombania nyota raia wa Ufaransa, Willem Geubells ambaye anaichezea klabu ya Olympique Lyon ya nchini Ufaransa. Nyota huyo mwenye miaka 16 anatajwa kutakiwa na Chelsea huku akitakiwa pia na vilabu vikubwa barani ulaya ikiwemo klabu ya Barcelona.

Taarifa zilizopo ni kwamba nyota huyo amekataa kusaini mkataba wa muda mrefu wa kuendelea kusalia kwenye klabu hiyo ya nchini Ufaransa ambapo mkataba wake wa sasa unaisha mwezi Juni mwaka huu.

Sababu kubwa ya nyota huyo kukataa kusaini mkataba mpya klabuni hapo inatajwa ni kutokana na kutaka kuhakikishiwa kucheza katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo lakini pia ikitajwa kutakiwa kwake na vilabu vikubwa kunamfanya atake kuachana na klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment