PSG WAANZA MIPANGO YA KUMNASA CONTE - Darajani 1905

PSG WAANZA MIPANGO YA KUMNASA CONTE

Share This
Darajani 1905 iliwai kuleta ripoti juu ya kocha wa Chelsea, Antonio Conte atakavyokuwa kwenye maiwndo na viongozi wa klabu ya PSG wakimtaka ajiunge na klabu hiyo mara baada ya kocha wa sasa kushindwa kuivusha klabu hiyo katika mafanikio yake ambayo klabu hiyo ilipanga kuyafikia kabla ya msimu ambapo taarifa zinadai kuwa klabu hiyo ilikuwa ikitazamia kushinda taji la klabu bingwa barani Ulaya mabpo juma hili wameshuhudia wakitupwa nje ya michuano hiyo dhidi ya Real Madrid. ambapo kutokana na matokeo hayo tukaamini kuwa itamaanisha sasa kocha Antonio Conte atakuwa amefunguliwa milango kutimkia klabuni hapo. Kusoma taarifa hiyo, bonyeza hapa

Na leo kuna gazeti la nchini Ufaransa, nch inayopatikana klabu hiyo ya PSG limeripoti kuwaklabu hiyo imeanza mawasiliano na kocha Antonio Conte ili ajiunge na klabu hiyo katika dirisha kubwa la usajili.

Gazeti hilo linaripoti kuwa klabu ya PSG haimtazamii tena kocha wake wa sasa, Unai Emery ukuendelea kubaki klabuni hapo na badala yake wameanza mawasiliano ili kumnyakua kocha Antonio Conte ili akaungane na klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment