MSIKIE MBAPPE ALICHOKISEMA KUHUSU CHELSEA - Darajani 1905

MSIKIE MBAPPE ALICHOKISEMA KUHUSU CHELSEA

Share This
Klabu ya Chelsea imewai kutajwa kumfukuzia nyota raia wa Ufaransa, Kylian Mbappe ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya PSG inayopatikana nchini humo huku kukiwa na mipango ya kumsajili kabisa ifikapo dirisha kubwa la usajili ambapo nyota huyo anatajwa kuigharimu PSG kiasi cha paundi milioni 160.

Je unajua kama nyota huyo alishawai kuichezea Chelsea?
Najua labda ulikuwa unahisi kwamba aliwai kuwa shabiki wa Chelsea tu na sio kuichezea labu hiyo haswa mara baada ya kuwai kuzagaa kwa picha zikimuonyesha akiwa na fulana ya Chelsea, haswa picha hizo zikisambaa kipindi kile akiwa na klabu ya As Monaco ambapo Chelsea ilitajwa kwa karibu kumfukuzia.

"Nilikuwa mdogo kipindi iko nikiwa na miaka 10 au 11, nilisafiri mpaka magharibi mwa jiji la London ambapo huko nilifanya mazoezi kwenye klabu ya Chelsea, kwenye akademi ya timu hiyo. Nakumbuka kuna mchezo tulicheza huku mi nikicheza kama mshambuliaji wa kati, na tukafanikiwa kushinda magoli 6-0 au 7-0 dhidi ya Charlton Athletic, lakini sikumbuki kama mi nilifunga"

"ulikuwa ni wakati mzuri kwangu, kucheza soka langu Uingereza, lilikuwa ni jambo la kuvutia" alisema kinda huyo ambaye kwa sasa ana miaka 19 na tayari ameshaonekana kuwa bora mpaka kuingia kwenye kikosi cha timu ya taifa akiwa anacheza kwenye ubora akiwa na klabu ya PSG.

Je unamuona Mbappe akiwa Chelsea siku moja?



No comments:

Post a Comment