MORATA AISHAWISHI CHELSEA IMSAJILI ASENSIO - Darajani 1905

MORATA AISHAWISHI CHELSEA IMSAJILI ASENSIO

Share This
Nyota wa klabu ya Real Madrid, Marco Asensio amekuwa akitajwa kutakiwa na klabu ya Chelsea, ambapo nyota huyo anatajwa kuwaambia viongozi wa klabu yake kwamba anataka nafasi ya kucheza zaidi kikosini apo ili aendelee kubaki kwenye klabu hiyo wa nchini Hispania.

Mara baada ya tetesi hizo, mhispania mwenzake klabuni Chelsea ambaye waliwai kucheza timu moja, Alvaro Morata natajwa kuishauri klabu yake ya Chelsea imsajili nyota huyo mwenye miaka 23 kwa sasa akisema kama Chelsea itafanikiwa kumnasa nyota huyo atakuwa chachu ya mafanikio klabuni Chelsea kutokana na ubora wake.

Nyota huyo ambaye alitua Chelsea kwenye dirisha kubwa la usajili ambapo alitua Chelsea kwa dau la paundi milioni 60 na sasa anaishawishi klabu hiyo imsajili mhispania huyo ili atue klabuni Chelsea.

Nyota huyo anatajwa kuwa na thamani ya euro milioni 150 (Tanzania shilingi  bilioni 417) huku mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich akitajwa kuvutiwa na nyota huyo.

No comments:

Post a Comment