HONGERENI WANAWAKE DUNIANI KOTE - Darajani 1905

HONGERENI WANAWAKE DUNIANI KOTE

Share This
Leo ni siku ya wanawwake duniani, nasi kama Darajani 1905 hatutoruhusu kupitwa na siku muhimu kama hii bila kusema asante kwa akina dada zetu na mama zetu na wanawake wote duniani maana bila wao wengi wengi kama sio wote tusingefika hapa tulipo bila wao. Nasi kwa kuwa ni Darajani 1905 ni ukurasa kwa ajili ya klabu ya Chelsea ambamo ndani yake pia kuna klabu ya wanawake ya Chelsea Ladies inayoshiriki ligi kuu kwa wanawake ya nchini Uingereza huku ikiwa kileleni mwa ligi hiyo lakini pia ikiendela kushiriki ligi mbalimbali.

Basi hapa nakuletea historia fupi ya klabu hiyo ilianzishwa lini na mpaka leo kufikia na mafanikio yake.

Chelsea Ladies kiuhalisia ilianzishwa mwaka 1992 ingawa ilikubalika na klabu kuu ya Chelsea Fc ili iwe klabu chini yao katika mwamvuli wa Chelsea Fc mwaka 2004, mara baada ya kufanikiwa kukubalika kuwa chini ya klabu ya Chelsea, klabu hiyo ya wanawake ikafaikiwa kupanda daraja na kuingia daraja la kwanza au daraja kuu la ligi ya wanawake huku ikiibuka kuwa mabingwa.

Ulishawai kujiuliza ni uwanja gani maalumu kwa ajili ya klabu hiyo? je nayo inautumia uwanja wa Stamford Bridge kama uwanja wake maalumu?

Jibu ni hapana, klabu hiyo haitumii uwanja wa Stamford Bridge ila inautumia uwanja wa Kingsmeadow ambao unapatikana huko Kingston Upon Thames ambapo uwanja huo unaingiza watazamaji 4,850 huku wanaokaa ni 2,265.

Timu hiyo imepata mafanikio makubwa ambapo mpaka sasa imefanikiwa kushinda mataji 13 ambapo taji la ligi kuu kwa wanawake (FA WSL 1) wameshinda mara moja, FA WSL Spring Series na FA Women's cup na Premier League Southern Division yote mara mojamoja wakati taji la Surrey County Cup wakishinda mara tisa.

Hongereni wanawake wote duniani..

No comments:

Post a Comment