MMILIKI ASEMA CONTE ATABAKI CHELSEA KWA SHARTI MOJA - Darajani 1905

MMILIKI ASEMA CONTE ATABAKI CHELSEA KWA SHARTI MOJA

Share This

Asubuhi ya leo kuna taarifa imechapishwa na gazeti la The Sun la  nchini Uingereza kuwa kocha wa Chelsea, Antonio Conte anaweza akaendelea kubaki kuwa kocha wa klabuni hapo, ila kwa sharti moja.

Inatajwa kwamba mmiliki wa klabu hiyo amemwambia kumaliza ndani ya klabu nne za juu katika msimamo wa ligi kuu Uingereza haitomfanya kocha huyo aendelee kubaki kuwa kocha wa klabu hiyo, ila ni jambo moja tu ndo linaweza kumfanya akaendelea kuwa kocha wa Chelsea.

Inaelezwa kwamba mmiliki huyo amemwambia kocha huyo kwamba ili aendelee kubaki hapo basi aache kulalamika au kuongelea vibaya mtindo au mfumo wa usajili unavyofanyika klabuni hapo ambapo sauti ya mwisho ipo katika bodi ya timu ambayo yenyewe ndiyo inashughulika na usajili klabuni hapo.

Kocha huyo amekuwa akikaririwa kulalamika juu ya usajili unavyofanyika klabuni hapo huku mara kadhaa akikiri kuwa alimtaka mchezaji flani ilo bodi imeshindwa kumsajili huku katika mkutano wake wa mwisho akionyesha dhahiri jinsi mfumo wa klabu ya Manchester city katika usajili anavyoupenda na kuutamani.

No comments:

Post a Comment