ANTONIO CONTE AMEKUWA 'BUBU' GHAFLA - Darajani 1905

ANTONIO CONTE AMEKUWA 'BUBU' GHAFLA

Share This

Klabu ya Chelsea imekuwa haina mfululizo mzuri wa matokeo mazuri katika michezo yake ya hivi karibuni, hali inayotajwa kumfanya kocha wa klabu hiyo, Antonio Conte kuonekana kuwa na maisha mafupi klabuni hapo huku baadhi ya vilabu vikitajwa kuvutiwa na kocha huyo ambaye anatajwa kuachana na Chelsea mwishoni mwa msimu huu.

Mara baada ya kutokea matokeo hayo ambapo michezo miwili iliyopita ambayo kocha Antonio Conte ameiongoza klabu hiyo yote ameshuhudia Chelsea ikipoteza huku ikitupwa nje katika klabu nne za juu katika msimamo wa ligi kuu.

Ambapo hiyo inatajwa kumfanya kocha huyo kuwa 'bubu' na kukata mawasiliano kwa viongozi wa Chelsea ambao wanaongea kiingereza na sio kiitaliano kama yeye.

Inaelezwa kuwa kocha huyo amekata mawasiliano na ukaribu baina yake na viongozi wote klabuni Chelsea wanaoongea kiingereza na badala yake anatajwa kuwa na mawasiliano na kaka yake tu ambaye alifika nae klabuni hapo pindi alipotambulishwa rasmi kuwa kocha wa Chelsea.

Sababu inayodhaniwa kwamba huenda kukata mawasiliano na viongozi hao ni kutokana na kutaka kuwa sawa na kuwa na maamuzi yake binafsi katika kipindi iki ambapo klabu haina mwenendo mzuri.

No comments:

Post a Comment