CHELSEA YAMSAINISHA NYOTA WAKE MKATABA MPYA - Darajani 1905

CHELSEA YAMSAINISHA NYOTA WAKE MKATABA MPYA

Share This

Klabu ya Chelsea kwa upande wa akina dada maarufu kama Chelsea Ladies mchana wa leo imefanikiwa kumsainisha mkataba mpya nyota wake Deanna Cooper ambaye anacheza nafasi ya ulinzi wa kati.

Nyota huyo aliseajiliwa na Chelsea akitokea klabu ya London Bees miezi 12 iliyopita alisajiliwa na Chelsea ingawa hakuwa na msimu mzuri mara baada ya kukaa nje kwa muda mrefu akiuguza majeraha yake, amesaini mkataba mpya leo mchana huku akipewa ofa ya miaka miwili zaidi ya kuitumikia Chelsea Ladies.

Mara baada ya kusaini mkataba huo, mwanadada huyo mwenye miaka 24 alipohojiwa juu ya nini anakiwaza mara baada ya kusaini mkataba huo alisema "Kiukweli nimefurahishwa kuwa moja ya timu inayoelekea mafanikio, najivunia kuwa hapa".

No comments:

Post a Comment