KOCHA ASEMA "BATSHUAYI ALISTAHILI KUJIUNGA NA BORRUSIA" - Darajani 1905

KOCHA ASEMA "BATSHUAYI ALISTAHILI KUJIUNGA NA BORRUSIA"

Share This
Klabu ya nchini Ujerumani, Borrusia Dortmund imekuwa ikitajwa kuifukuzia saini ya nyota wa Chelsea, Michy Batshuayi ambaye anaichezea kwa mkopo klabu hiyo. Klabu hiyo imekuwa ikiripotiwa kuwa na nia ya kutaka kuendelea kumbakisha nyota huyo mwenye miaka 24 ili atumike kama mshambuliaji chaguo la kwanza katika kikosi hicho kinachoshiriki ligi kuu nchini Ujerumani maarufu kama Bundesliga.

Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya kinda huyo mwenye miaka 24, timu ya taifa ya Ubelgiji, Marc Wilmots anaamini nyota huyo anastahili kuendelea kubaki kwenye klabu hiyo ya nchini Ujerumani kutokana na aina yake ya uchezaji na jinsi anavyopata muunganiko mzuri klabuni hapo.

"Aina ya uchezaji ya Borussia inaendana sana na aina yake ya uchezaji. katika hali ya mchezo wamekuwa wakimfanya mchezaji aendane na hali ya kimchezo na hata kisoka kuwa vizuri, ambapo kwa maana hiyo itamfanya Batshuayi azidi kuwa bora na kupata changamoto mpya. Anaweza pia akajiongeza kutokana na aina ya ushambuliaji inayotumika klabuni pale"

"Wanatumia haswa mipira mirefu, lakini wamekuwa vizuri pia kuumiliki mpira katika eneo la adui na kusababisha madhara. Uamuzi wake wa kujiunga na Borrusia lilikuwa ni jambo sahihi kulifanya. Kila goli analolifunga limekuwa na faida kwa kila klabu anayoichezea"

"jambo zuri ni kwamba, kila anapopata nafasi ya kuwa kwenye klabu fulani, anakuwa ni mtu mwenye furaha muda wote na anatakiwa kucheza timu ambayo ana uhakika wa kucheza kila mchezo. Lakini hakuna anayejua kipi kitatokea mara baada ya miezi minne" alisema kocha huyo.

Chelsea inaweza kuungana na nyota huyo mwishoni mwa msimu ambapo ndio mkataba wake wa mkopo utakapomalizika toka kujiunga na klabu hiyo katika dirisha dogo la usajili la mwezi Januari alipojiunga na klabu hiyo mara baada ya klabu hiyo kuachana na mshambuliaji wake, Emerick Aubameyang.

No comments:

Post a Comment