CHELSEA KUMFUATA TENA NYOTA KUTOKA REAL MADRID - Darajani 1905

CHELSEA KUMFUATA TENA NYOTA KUTOKA REAL MADRID

Share This
Chelsea iliwai kuhusishwa na nyota wa kikosi cha vijana cha Real Madrid, Oscra Rodriguez katika dirisha dogo la usajili lililopita la mwezi Januari, ingawa usajili huo ukaaishia mitini. Lakini sasa Chelsea inatajwa kuanza mipango yake ya chini kwa chini ya kumsajili nyota huyo kutoka klabuni hapo mwenye miaka 19 kwa sasa.

Oscar Rodriguez amekuwa akikichezea kikosi cha Real Madrid ya vijana huku akitajwa kuwa na sifa na uwezo mkubwa kama gwiji wa zamani wa Chelsea, Frank Lampard ambapo mpaka sasa amefanikiwa kuichezea Real Madrid ya wakubwa mchezo mmoja tu kwenye kombe la Copa del Ley anatajwa kuingia kwenye anga za Chelsea haswa kuelekea kwenye dirisha hili kubwa la usajili mwishoni mwa msimu.

Nyota huyo anamalizana na klabu hiyo mwezi Juni mwaka huu ambapo Chelsea kama ikimtaka itaweza kumpata bure kutokana na mkataba wake kumalizika katika mwezi huo mwaka huu na bado mpaka sasa Real Madrid hawajampa mkataba mpya.

No comments:

Post a Comment