KITAMBO; UNAIKUMBUKA HII? CHELSEA NA MIAMVULI UWANJANI - Darajani 1905

KITAMBO; UNAIKUMBUKA HII? CHELSEA NA MIAMVULI UWANJANI

Share This
Chelsea itasafiri mpaka nchini Hispania kucheza dhidi ya Barcelona katika mchezo wa klabu bingwa barani Ulaya siku ya jumatano, ambapo mchezo huo utakuwa ni mchezo wa marudiano kwa hatua ya 16 bora kwa klabu hizo ambapo mchezo wa kwanza uliochezwa Stamford Bridge uliisha kwa sare ya 1-1 huku Willian akiwa mfungaji wa goli la Chelsea.

Kuelekea kwenye mchezo huo, hapa nataka nikukumbushe moja ya michezo ambayo Chelsea ilisafiri katika michuanoo hiyo ikiifata klabu ya Besiktas ili kucheza mchezo wake wa hatua ya makundi ambapo ulikuwa mchezo wa kundi G, hiyo ilikuwa mwaka 2003.

Mchezo wa kwanza baina ya timu hizo ulichezwa kwenye uwanja wa Stamford Bridge na wakati huo Chelsea ilitakiwa kuifata Besiktas ili kucheza mchezo wake wa marudiano, kumbuka Besiktas inapatikana kwenye nchi ya Uturuki ambayo umbali wake wa kutoka Uingereza mpaka nchini humo, ni mwendo kama wa masaa 40 kwa ndege.

Siku kadhaa kabla ya Chelsea kusafiri kucheza mchezo wake huo wa hatua ya makundi nchini Uturuki kulitoa shambulio la kigaidi ambapo bomu lililipuliwa na kuua zaidi ya watu 50 ambapo kutokana na wasiwasi wa kiusalama ikaamriwa mchezo huo kati ya Chelsea dhidi ya Besiktas uhamishwe na kutolewa nchini humo ambapo baadae ukapangwa kuchezeka kwenye nchi ya Ujerumani ambapo umbali wake kutokea Uturuki ni kama kilometa 2,000.

Lakini hiyo haikuwa sababu ya mashabiki lukuki wa Besiktas kusafiri na kuungana na klabu yao ili kuishangilia katika mchezo huo wa marudiano huku mchezo wa kwanza uliisha kwa Chelsea kushinda mabao 2-0.

Mchezo huo ukapangwa kuchezeka kwenye uwanja wa Schalke 04, klabu inayopatikana nchini Ujerumani na mashabiki wa Besiktas walikuwa wengi ambapo wengi wao wakitoka nchini Ujerumani lakini na wengine wakisafiri kuufata mchezo huku jambo kubwa likishuhudiwa mashabiki wa Galatasaray, ambayo ni klabu adui wa Besiktas nao wakaungana kwa pamoja na maadui zao na kuishabikia Besiktas kwa pamoja.

Chelsea iliingia uwanjani huku ikiwakosa nyota wake kama Hernan Crespo, Adrian Mutu na Eidur Gudjohnsen huku ikimtumia Jesper Gronkjaer akicheza sambamba na Jimmy Floyd Hasselbaink katika safu ya ushambuliaji huku kocha wa Chelsea kipindi iko, Claudio Ranieri akitumia mfumo wa 3-5-2. Lakini kabla ya mchezo kuanza kuna tukio lilitokea ambapo mashabiki wa Besiktas ambao walichanganyika na mashabiki wa Galatasaray walitupa fataki na uchafu mwingi katika eneo la uwanja huku ikitajwa sababu kubwa ni kuonyesha hasira zao kwa mchezo huo kuamishwa kutoka kuchezeka nchini kwao Uturuki na kupelekwa nchini Ujerumani hali iliyosababisha benchi la ufundi la Chelsea kutumia miamvuli ili kujikinga na fataki hizo zilizokuwa zinarushwa.

Mchezo ukachezeka na Chelsea ikafanikiwa kushinda ushindi wa mabao 2-0, magoli yakifungwa na Hasselbaink na Wayne Bridge na kufanikiwa kufudhu katika hatua hiyo ya makundi huku Besiktas akimaliza nafasi ya tatu katika kundi hilo.

No comments:

Post a Comment