ANTONIO CONTE AFUNGULIWA MILANGO KUTUA PSG - Darajani 1905

ANTONIO CONTE AFUNGULIWA MILANGO KUTUA PSG

Share This
Usiku wa jana klabu ya nchini Ufaransa, PSG ilitupwa nje ya mashindano au michuano ya klabu bingwa barani Ulaya mbele ya Real Madrid kwa kufungwa mabao jumla 5-2 na mabingwa watetezi hao wa ligi hiyo, mara baada ya kutupwa nje ya kichuano hiyo ambayo inaaminika ndiyo michuano iliyoifanya klabu ya PSG itumie dau kubwa kwenye usajili ili iweze kulitwaa taji hilo kwa muda mrefu sasa.

Kwa hivyo, kama imeshindwa kufanikiwa lengo lake basi inaaminika kocha wa klabu hiyo, Unai Emery atakuwa hana kibarua tena klabuni hapo, ambapo klabu ya PSG itamtimua kwa kushindwa kutimiza lengo, na kufukuzwa kwa kocha huyo kutamaanisha klabu hiyo itaingia sokoni kumtafuta kocha mwenye uzoefu na michuano hiyo lakini pia mwenye mafanikio makubwa kwenye ngazi ya kuishindani na ndio hapo itamtolea macho kocha wa Chelsea, Antonio Conte ambaye alishawai kutajwa kutakiwa na klabu hiyo sambamba na kocha wa sasa wa Manchester united, Jose Mourinho.

Lakini itakuwa ngumu kumnasa Mourinho maana ametoka kusaini mkataba mpya klabuni Manchester ambapo atakuwa klabuni hapo mpaka mwaka 2020, ambapo hiyo inamaanisha kocha Antonio Conte atakuwa kwenye makucha ya matajiri wa PSG ili atue klabuni hapo.

"PSG watataka kuanza tena kampeni yao ya kushinda klabu bingwa. Tumeshaona tayari kwamba kushinda klabu bingwa sio kazi rahisi, na huwezi kutoa pesa kulinunua taji hilo. Watatakiwa kuingia sokoni kumtafuta kocha bora zaidi ya Unai Emery" alisema mchambuzi Julian Laurens

"Nafikiri mmiliki ana orodha ya makocha anaowatazamia. Mtu kama Antonio Conte na Mauriccio Pochettino naamini wapo kwenye orodha hiyo. Lakini pia kuna Luis Enrique pamoja na Allegri. Ni klabu kivutio kwa kila kocha"

Alipoulizwa kama anadhani Jose Mourinho ataweza kujiunga na klabu hiyo alisema "Walishajaribu kumsajili lakini Man utd kumpa mkataba mpya, inamaanisha itakuwa haiwezekani kumnasa"

No comments:

Post a Comment