NYOTA WATFORD AZIDI KUITAMANISHA CHELSEA - Darajani 1905

NYOTA WATFORD AZIDI KUITAMANISHA CHELSEA

Share This
Chelsea ilikuwa ni klabu mojawapo iliyowai kumtaka nyota Richarlison pindi alipokuwa akiichezea klabu ya Fluminense ya nchini Brazil ambapo ndipo alipozaliwa na kukulia huko, na ni mchezaji wa nchi hiyo lakini baadae akajiunga na klabu ya Watford ambayo alijiunga nayo katika dirisha kubwa la usajili la kipindi cha kiangazi.

Nyota huyo akajiunga na klabu hiyo huku akipewa mshahara wa paundi 20,000 kwa wiki huku akipewa mkataba wa miaka mitano. Licha ya kujiungta na klabu hiyo lakini bado haijawazuia Chelsea kujaribu kumsajili tena, na nyota huyo ametoa neno kutokana na kutakiwa kwake na vilabu vikubwa barani Ulaya haswa Chelsea ikionekana kuongoza orodha hiyo ya kumtaka nyota huyo.

"Kiukweli kwa sasa natazamia kucheza na mawazo yangu yakiwa kwa Watford tu, ingawa nitatamani pia kucheza ligi ya mabingwa Ulaya na hata kuibuka mffungaji bora wa ligi kuu" alisema nyota huyo ambaye kwa sasa ana miaka 20.

Nyota huyo mara kadhaa amekuwa akikaririwa akisema ana ukaribu na nyota wa Chelsea, David Luiz pamoja na Willian ambao amekuwa akienda nyumbani kwao na kushinda nao pamoja siku za mapumziko.

No comments:

Post a Comment