USAJILI WA ISCO KUTUA CHELSEA, MORATA KUHUSIKA - Darajani 1905

USAJILI WA ISCO KUTUA CHELSEA, MORATA KUHUSIKA

Share This

Chelsea imekuwa ikihusishwa kufanya biashara na Real Madrid, huku wachezaji kupishana katika biashara hiyo ndicho kitu kinachotajwa kutokea, nyota wa Chelsea, Eden Hazard anatajwa kutaka kujiunga na klabu ya Real Madrid, lakini pia Marco Asensio na Isco wote wa Real Madrid wanatajwa mmojawapo kujiunga na Chelsea, iwe kwa kufanyika mabadilishano ama Chelsea imsajili mmojawapo kwa dau nono la pesa.

Wakati tetesi hizo zikiwa zinaendelea, gazeti moja la nchini Hispania ambapo ndipo inapotokea timu hiyo pamoja na nyota wake hao wawili limeripoti kuwa Chelsea ina nafasi kubwa ya kumnasa Isco kutoka Real Madrid kutokana na mahusiano na urafiki uliopo kati ya nyota huyo na nyota wa Chelsea, Alvaro Morata.

Gazeti hilo liliitaja Manchester city ambao nao wanamtaka nyota huyo mwenye miaka 25 kwamba kama wanamtaka Isco basi itawalazimu wamsajili Alvaro Morata ili aungane na klabu hiyo ndipo itakuwa rahisi kwa klabu hiyo kumnasa Isco.

Isco na mke wake waliwai kusafiri na kufika kwenye jiji la London ambapo hapo walikutana na Alvaro Morata pamoja na mke wake Alice Campelo ambapo hiyo ilionyesha kuwa kama Chelsea ikiamua kumtumia Morata basi itakuwa na kazi ndogo ya kumshawishi.

No comments:

Post a Comment