NATHAN AKE ASHINDA TUNZO NYENGINE - Darajani 1905

NATHAN AKE ASHINDA TUNZO NYENGINE

Share This
Nyota wa zamani wa klabu ya Chelsea, Nathan Ake ambaye aliondoka klabuni Chelsea na kujiunga na klabu ya Afc Bournemouth ambayo inashiriki ligi kuu Uingereza kama Chelsea amefanikiwa kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Februari klabuni huko alipo.

Nyota huyo amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Februari  ikiwa ni tunzo ya tano toka ajiunge na klabu hiyo katika dirisha kubwa la usajili lililopita mara baada ya kujiunga na klabu hiyo kwa mkopo kabla ya baadae kuuzwa kabisa.

Nathan Ake ambaye ni raia wa Uholanzi alijiunga na Bournemouth kwa dau la paundi milioni 20 amefanikiwa kushinda tunzo hiyo huku akiwa mchezaji bora pia kwa miezi ya Agosti, Oktoba, Novemba, Desemba na leo mwezi Februari.

No comments:

Post a Comment