Chelsea imepoteza mchezo wake muhimu dhidi ya Barcelona hapo jana, ambapo hiyo inamaanisha Chelsea imebakiza mataji mawili kama sio moja ya kugombania katika msimu huu, taji la kombe la FA ambapo itamenyana dhidi ya Leicester katika hatua ya robo fainali. Lakini licha ya kupoteza mchezo huo na kutupwa nje katika michuano hiyo ya klabu bingwa barani Ulaya, kuna mashambulizi mengi yametupwa kwa mlinda mlango wa Chelsea, Thibaut Courtois ambapo inadaiwa aliruhusu kufungwa magoli ya kizembe yaliyoigharimu Chelsea na kutufanya tupoteze mchezo huo.
Nyota huyo amejibu lawama hizo huku akikiri kufanya makosa.
"Makosa yetu wenyewe ndiyo yametugharimu katika michezo yote miwili (nyumbani na ugenini). Kwa goli la kwanza nilikuwa sijategemea kama Messi angeupiga ule mpira nami nilichelewa kufunga miguu kwa hiyo lilikuwa ni kosa nimelifanya. Kwangu haikuwa jambo zuri kuanza mchezo kwa mtindo ule. Mengine tulipoteza pasi nao wakatumia makosa yeu, ulikuwa ni uzembe wetu na makosa yetu, wakatuadhibu"
"Ukiachana na hilo, tulijilinda vizuri na tukajaribu kucheza soka safi na tulitengeneza nafasi za kufunga. Tuligongesha mwamba mara mbili, hatukuwa na bahati lakini makosa yetu wenyewe ndiyo yaliotuadhibu. Inatakiwa tuwe wakweli katika hilo, sasa inatakiwa tujiandae ili tuweze kupata ushindi katika mchezo ujao wa kombe la FA kwa maana hiyo ndiyo nafasi yetu pekee ya kushinda taji msimu huu"
COURTOIS AONGELEA MCHEZO DHIDI YA Barcelona
Share This
Tags
# Chelsea FC
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea FC,
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment